MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali katika uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 (Toleo la 2023) pamoja na Mfumo wa e-Ardhi, tukio lililofanyika leo Machi 17, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Uzinduzi huo, ukiwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, umehudhuriwa na wakurugenzi wa halmashauri kutoka kote nchini, huku kila mmoja akisisitiza umuhimu wa sera hii mpya katika usimamizi bora wa ardhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa sera ya Ardhi ya mwaka 1995 (Toleo la mwaka 2023) Jijini Dodoma (Picha na: Ikulu)
Kwa mujibu wa wataalamu wa ardhi, mfumo wa e-Ardhi unalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi kwa njia ya kidijitali, kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza uwazi katika utoaji wa hati miliki.
Katika mazungumzo yake Irafay, amesisitiza kuwa mabadiliko haya yatasaidia halmashauri katika kupanga matumizi bora ya ardhi na kuharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Sera hii inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya ardhi nchini, ikizifanya halmashauri kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wake ndani ya mipaka ya kiutawala.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.